Sunday, 29 January 2017
Saturday, 28 January 2017
Vita vyarejea tena Sudan ya Kusini
Mapigano yamerejea nchini Sudan Kusini kati ya serikali na waasi walio watiifu kwa aliyekuwa makamu wa rais nchini humo Riek Machar.
Ripoti kutoka kwa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Upper Nile zinasema kumekuwa na mapigano makali ndani na nje ya mji wa Malakal ,ambapo wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanawahifadhi watu walioachwa bila makao.
Msemaji wa jeshi amesema kuwa idadi ya watu waliojeruhiwa haijulikani kwa kuwa vita hivyo vinaendelea.
Umoja wa Mataifa umezitaka pande hasimu kusitisha uadui na kutekeleza makubaliano ya amani ya mwaka 2015.
Juhudi za kuwanusuru wachimbaji wadogo wa migodi waliofukiwa na Kifusi yaendelea vizuri, Kwa habari kamili Soma hapa
Amesema kwamba jana wamefanikiwa kufanya mawasiliano na wachimbaji hao na kwamba wapo kumi na watano na kuwa wanachohitaji kwa sasa ni chakula.
Alisema waokoaji walifanikiwa kuwafikishia kamba na kalamu watu hao ambao waliandika majina na mahitaji yao na kusema kwamba wote wapo salama.
Watu hao akiwemo raia wa China mmoja walifukiwa na kifusi juzi usiku baada ya udongo kukatika na kuziba mlango waliokuwa wakitumia kuingia na kutoka na uokoaji unaendelea kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya uokoaji.
Watu wengi wapo katika eneo hilo wakiwemo ndugu wa waliofukiwa lakini kwa juhudi wanazoziona za uokoaji wametulia na kufuata maelekezo wanayopewa ikiwemo kukaa mita 500 toka eneo la tukio.
Soma hapa ujumbe waliotuma
hata hivyo juhudi za kuwaokoa kutoka chini ya mgodi inaendelea vizuri ambapo matumaini ya kuwapata hai wote inaonekana
Subscribe to:
Comments (Atom)
MJMBA JAX
-
Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea iwapo kidonda cha ukubwa wa angalau wa nusu sentimita kitatokea kwenye sehemu yeyote ya ukuta wa tu...
-
Moja ya magonjwa hatari sana ambayo yanaweza kumpata mtu yoyote ni ugonjwa wa shambulizi la moyo. Huu ni miongoni mwa magonjwa yanayoo...























































